Mbappe Wa Zanzibar Asaini Singida Black Stars
MLANDEGE inayoshiriki Ligi Kuu Zanzibar (ZPL), imetangaza kuachana na mshambuliaji wake, Mussa Hassan ‘Mbappe’ huku ikimtakia kheri katika safari yake mpya.
“Tunakupongeza kwa hatua yako mpya ya kujiunga na Singida, tunakutakia mafanikio makubwa katika kila hatua ya safari yako,” imeeleza taarifa hiyo.
Pia, ilitoa pongezi kwa mchezaji huyo kwa kujitoa, kupambana na kuipa klabu kila alichokuwanacho huku ikieleza mchango wake umeacha alama ambayo itabaki kuwa sehemu ya historia yao.
Soka La Bongo ilimtafuta mshambuliaji huyo kutaka kujua undani wa taarifa ya kujiunga na Singila.
“Mkataba wa kuitumikia Mlandege umeisha ila kwa upande wa Singida bado mambo hayajakamilika ndio maana nimekaa kimya,” amesemaMbappe
Mshambuliaji huyo alimaliza msimu wa 2025-2026 akifunga mabao tisa katika Ligi Kuu Zanzibar.