Singida Big Stars FC

Metacha Apewa Mitatu Singida Black Stars

Vardo July 14, 2026 8:07 pm

BAADA ya golikipa wa Singida Black Stars, Metacha Mnata kumaliza mkataba wake msimu ulioisha wa 2025-2026, imeelezwa kwamba uongozi wa timu hiyo umempatia mwingine wa miaka mitatu.

Chanzo cha kuaminika kutoka katika timu hiyo, kilisema Singida BS imemuongezea Metacha mkataba wa miaka mitatu, baada ya kuamini uwezo wake kama kipa mzawa.

“Ukitaja magolikipa wazawa wanaofanya vizuri, huwezi kuliacha nyuma jina la Metacha, ana uzoefu mkubwa wa michuano ya kimataifa, kulingana na majukumu ya msimu ujao tumeona huduma yake ni muhimu,” kilisema chanzo hicho na kuongeza;

“Kabla ya msimu mpya kuanza Agosti 14, mbele yetu tuna michuano ya Kombe la Cecafa Kagame 2026, hivyo lazima tuwe na wachezaji kama Metacha katika timu.”

Metacha ambaye msimu ulioisha alimaliza akiwa na cleansheets tano katika Ligi Kuu ya NBC, amewahi kucheza timu mbalimbali ikiwemo Yanga, Azam na Polisi Tanzania.
“Ukiachana na Metacha, kuna wachezaji wengine ambao wanaongezwa kikosini wenye uzoefu mkubwa watakaotusaidia kwenye michuano mbalimbali msimu ujao,” kilisema chanzo hicho.

Singida Black Stars baada ya kumaliza nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC, itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika kwa msimu wa pili mfululizo baada ya 2025-2026 kuishia makundi.

Singida ni miongoni mwa wawakilishi wa Tanzania katika mashi ndano ya Kagame, timu hiyo inakwenda kushiriki ikiwa bingwa mtetezi, ikiambana na Simba ambayo ni bingwa wa kihistoria ikishinda mataji sita. Pia kuna KVZ ya Zanzibar.

FIFA Yashusha Mpira Wa Mechi Nne JKT Tanzania Yachukua Kipa Mpya