Michezo

Vodacom Yadhamini Mashindano Ya Golf Ya Corporate Masters 2026

Vardo July 16, 2026 10:54 pm

Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Tanzania Plc, Joseph Sayi (katikati) akizungumza wakati wa kutangaza udhamini wa Mashindano ya Golf ya Vodacom Corporate Masters 2026, yaliyoandaliwa kwa ushirikiano na Lugalo Golf Club kwa lengo la kuunganisha jumuiya ya wafanyabiashara nchini Tanzania, kuimarisha mahusiano ya kibiashara, kukuza ushirikiano na kuleta fursa zenye tija kwa wateja, washirika wa kibiashara na wadau muhimu nchini. Mashindano hayo yatakayofanyika tarehe 1 Agosti 2026 yanaendelea kuimarisha nafasi ya Vodacom kama mshirika wa kuaminika katika teknolojia na huduma za mawasiliano kwa taasisi na mashirika yanayoendelea kukua katika mazingira ya uchumi wa kidijitali. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 16 Julai 2026 jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Katibu wa Corporate Masters, Maryanne Mugo (kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Corporate Masters, Ken Mbaya (kulia).

Vodacom Tanzania PLC Yazindua Mashindano Ya Golf Kuimarisha Uhusiano Wa Kibiashara Tanzania Ni Nafasi Nyingine Kwa Jonathan Sowah