Peter Shalulile Yanga
Yanga SC

Shalulile Atishika na Uzito wa Kariakoo Derby: “Simba na Yanga ni Tofauti!”

Vardo August 4, 2026 9:44 am

Mshambuliaji mpya hatari wa Yanga SC, Peter Shalulile, ameweka wazi kuwa tayari anazisikia na kuzihisi pigo za presha kubwa inayozunguka pambano la watani wa jadi, Kariakoo Derby, huku akisubiri kwa hamu kubwa kuingia uwanjani kuikabili Simba SC.

Shalulile, ambaye amesajiliwa hivi karibuni kuja kuongeza makali kwenye safu ya ushambuliaji ya Wananchi, anatazamiwa kucheza dabi yake ya kwanza kabisa nchini Agosti 12, 2026, wakati timu hizo zitakapokutana kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa katika Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar.

Nyota huyo wa kimataifa amefunguka kuwa tangu atue Tanzania, amekuwa akipokea simulizi na tahadhari nyingi kutoka kwa wachezaji na marafiki zake waliowahi kucheza Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League), wakimweleza kuwa Hakuna mechi inayobeba hisia na presha kubwa kama ya Simba na Yanga.

“Mara nyingi marafiki zangu wamekuwa wakiniambia kuwa mchezo wa Simba na Yanga una hisia za kipekee na presha kubwa kuliko mechi nyingi nilizowahi kucheza. Kadri siku zinavyosogea, ndivyo ninavyozidi kuusubiri kwa hamu kubwa,” alisema Shalulile.

Ameongeza kuwa kila anapofikiria kuhusu siku hiyo ya pambano, anajikuta akipata hamasa kubwa ya kuingia uwanjani, akiamini kuwa mechi hiyo ya Ngao ya Jamii itakuwa fursa bora kwake kujitambulisha rasmi na kuweka alama ya kwanza kwa mashabiki wa Yanga.

Mchezo huo wa Ngao ya Jamii visiwani Zanzibar unatarajiwa kuwa ndio ufunguzi rasmi wa msimu mpya wa soka nchini, ambapo mashabiki wa pande zote mbili watakuwa na shauku ya kuona kikosi gani kimejipanga vyema.

Aibu Au Mtego? Simba na Yanga Kuanzia Raundi ya Kwanza CAF Champions League 2026/27 Simba Yawatengea Azam Sh Bilioni 1.7 Kumvuta Fei Toto Msimbazi