Selemani Mwalimu Simba
Simba SC

Wydad Kumrudisha Selemani Mwalimu, Simba Yapewa Mtego Mpya Usajili

Vardo August 8, 2026 7:00 pm

Klabu ya Wydad Athletic Club ya nchini Morocco imeonyesha nia ya wazi ya kumrudisha nchini humo mshambuliaji wa Kitanzania, Selemani Mwalimu, ambaye kwa sasa anahusishwa na mpango wa kuendelea kuichezea Simba SC msimu ujao.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Simba kwa mkataba wa mkopo akitokea Wydad, na uwepo wake ndani ya kikosi cha Wekundu wa Msimbazi umeonekana kuongeza chachu na matumaini makubwa katika safu ya ushambuliaji.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na mtandao wa Felix Jason, uongozi wa Wydad umepokea na kuifanyia kazi ofa ya Simba inayotaka kumsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa permanent (wa kudumu). Hata hivyo, miamba hiyo ya Soka Morocco haijaonyesha nia ya kumwachia kirahisi mshambuliaji huyo chipukizi.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa pande zote mbili zipo kwenye mazungumzo na “kila kitu kipo mezani, muda wowote mambo yatakamilika.” Pamoja na hayo, Wydad bado ina kipengele kinachowapa nafasi ya kumrejesha Mwalimu iwapo masharti ya Simba hayatatimia.

Kiwango kizuri alichokionyesha Mwalimu akiwa na jezi ya Simba kimeifanya klabu hiyo ya Msimbazi kupambana kuhakikisha inapata saini yake ya kudumu kabla ya msimu mpya wa 2026/27 kuanza.

Hivi sasa sakata hilo limeingia kwenye hatua ya vutuvute, huku uongozi wa Simba ukitakiwa kufanya maamuzi ya haraka na ya busara ili usimpoteze nyota huyo ambaye bado ana mkataba wa muda mrefu na Wydad Athletic Club.

Kocha Barker Athibitisha Kurejea kwa Neo Maema Simba SC Simba Queens Yaitambulisha Safu Mpya Simba Day: Mgosi Aongoza Jahazi!