Hatma ya Depu Yanga: Aachwa Kikosi cha Wiki ya Mwananchi 2026/27?
Mshambuliaji wa Yanga, Laurindo Depu, anaonekana kuingia kwenye sintofahamu kubwa kuhusu hatma yake ndani ya klabu hiyo baada ya jina lake kutotajwa wakati wa utambulisho wa kikosi cha msimu wa 2026/27.
Tukio hilo lilijiri katika kilele cha Tamasha la Wiki ya Mwananchi lililofanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ambapo maelfu ya mashabiki walihudhuria kushuhudia nyota watakaowakilisha Wananchi msimu mpya.
Akitaja majina ya wachezaji watakaounda kikosi hicho, Afisa Habari na Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, alitaja orodha ndefu ya nyota wa zamani na wapya, lakini jina la Depu halikuwemo kabisa. Hatua hiyo imeibua maswali mengi miongoni mwa mashabiki, ikiashiria kuwa huenda mshambuliaji huyo hayupo kwenye mipango ya mwalimu kwa msimu ujao.
Kikosi Kilichotambulishwa:
-
Makipa: Diarra Djigui, Abdultalib Mshery, Hussein Masalanga.
-
Mabeki: Bakari Mwamnyeto, Dickson Job, Shadrack Boka, Ibrahim Bacca, Kouassi Yao, Kibwana Shomari, Nickson Kibabage, Erick Mwijage, Denis Nkane.
-
Viungo: Mudathir Yahya, Abdulnassir Abdallah, Mohammed Mussa, Abubakar Nizar, Farouk Komara, Duke Abuya, Allan Okello, Aziz Andambwile, Edmund John, Mohammed Hussein, Aboubakary Salum.
-
Washambuliaji: Max Nzengeli, Fred Ngoma, Peter Shalulile, Ibrahima Touré, Albert Kangwanda, Housseine Zakouani, Clement Mzize, Mohammed Damaro, Issa Abushiri.
Suala la Pacome Zouzoua Nalo Laibua Maswali
Mbali na Depu, kiungo mshambuliaji machachari Pacome Zouzoua naye hakutajwa kwenye kikosi hicho. Hata hivyo, tofauti na Depu, kukosekana kwa Pacome kunahusishwa moja kwa moja na majeraha ya muda mrefu yanayomsumbula, ambapo taarifa zinaeleza kuwa anaweza kukosa sehemu kubwa au msimu mzima wa 2026/27 akipatiwa matibabu.
Je, Depu Ataonyeshwa Lango la Kutokea?
Kwa upande wa Laurindo Depu, uongozi wa Yanga haujatoa taarifa rasmi kueleza sababu za jina lake kuachwa nje. Mashabiki na wadau wa soka sasa wanasubiri kwa hamu ufafanuzi kutoka kwa mabosi wa klabu hiyo ili kubaini kama mchezaji huyo ataolewa kwa mkopo, kuvunja mkataba, au kusajiliwa timu nyingine kabla ya dirisha la usajili kufungwa.