WAFCON 2026 Mchujo wa Kombe la Dunia
Habari za michezo

Vita Ya Tiketi Ya Kombe La Dunia: Nigeria, Afrika Kusini, Ghana Na Ivory Coast Kukiwasha Leo WAFCON

Vardo August 13, 2026 8:44 am

BAADA ya kushuhudia mechi za nusu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wanawake (WAFCON), leo msisimko unahamia kwenye hatua ya mtoano ambapo timu nne zitamenyana vikali kwenye viwanja tofauti kusaka fursa ya kufuzu Kombe la Dunia la Wanawake 2027 nchini Brazil.

Katika mchezo wa kwanza wa WAFCON 2026 mchujo wa Kombe la Dunia, Ivory Coast itakuwa nyumbani kuikaribisha Ghana kuanzia saa 2:00 usiku katika Uwanja wa Larbi Zaouli. Hii ni vita halisi ya Afrika Magharibi inayokutanisha Ivory Coast, iliyonyesha kiwango bora mashindanoni mwaka huu, dhidi ya Ghana yenye uzoefu na historia kubwa kwenye soka la wanawake barani Afrika.

Kibarua kingine kizito kitakuwa saa 4:00 usiku katika Uwanja wa Moulay Rachid, ambapo mabingwa wa zamani Afrika Kusini watavaana na miamba Nigeria. Timu hizi mbili zilizoondolewa kwa mshtuko katika hatua ya robo fainali—Nigeria ikifungwa na Cameroon huku Afrika Kusini ikiangukia pua 1-2 dhidi ya Morocco—sasa zinakutana kwenye vita ya kusaka nafasi ya mchujo wa mabara.

Mshindi wa mechi hizi za leo atapata tiketi ya kuingia kwenye mchujo wa mabara (inter-confederation play-offs), ambapo wawakilishi wa Afrika watamenyana na timu kutoka Asia, Marekani na mabara mengine ili kusaka nafasi za mwisho kuelekea Brazil.

Makocha Wanenavyo:

  • Justine Madugu (Kocha wa Nigeria): “Tunatambua wazi kuwa hii ni moja ya mechi ngumu zaidi kwetu, lakini hatuna chaguo lingine zaidi ya kupambana hadi mwisho ili kuwania nafasi hii ya mwisho.”

  • Kim Lars (Kocha wa Ghana): “Tuna imani kubwa kuwa bado tuna nafasi ya kufanya vizuri kwenye mchezo wa leo, ingawa tunajua haitakuwa rahisi kutokana na ubora wa mpinzani wetu.”

Said Mussa Mbeki Ajiunga na KVZ: Sababu za Kuondoka Mlandege na Mipango Mipya Sakata la Selemani Mwalimu: Pigo la Saikolojia Simba, Neema Yanga