PSG Kuaanza Kutetea Taji la UCL Mbele ya Slovan Bratislava
Paris Saint-Germain inaanza kampeni yake ya kutetea ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kuikaribisha Slovan Bratislava katika dimba la Parc des Princes. Mchezo huo utapigwa leo Jumatano, Septemba 9, saa 22:00 usiku, ukiwa ni mchezo wa kwanza wa hatua ya ligi.
PSG inaingia ikiwa na presha kubwa ya kuanza kwa ushindi mbele ya mashabiki wake, hasa baada ya kutwaa taji la Ulaya na kutaka kuendeleza ubabe wake katika michuano hiyo.
Hata hivyo, PSG haijaanza msimu wa ligi ya Ufaransa kwa kiwango kilichotarajiwa. Timu hiyo haijapata ushindi katika mechi zake tatu za mwanzo za Ligue 1, huku ikipoteza 2-1 dhidi ya Monaco katika mchezo wake wa mwisho.
Kocha Luis Enrique bado anaamini kikosi chake kina uwezo wa kurejea kwenye kiwango bora, na Champions League inaweza kuwa nafasi nzuri ya kubadilisha hali hiyo.
Kwa upande wa Slovan Bratislava, timu hiyo haitakiwi kuingia uwanjani ikiwa tayari imekubali kushindwa. Wawakilishi hao wa Slovakia wameonyesha uwezo wa kupata matokeo mazuri katika baadhi ya michezo yao, ingawa wameingia kwenye mchezo huu baada ya kupoteza mechi mbili za mwisho za ndani. Changamoto kubwa kwao itakuwa kuhimili presha ya PSG, hasa ikiwa wenyeji wataamua kucheza kwa kasi tangu dakika za mwanzo.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Kimbinu, PSG inatarajiwa kutawala mpira na kutumia kasi ya washambuliaji wake pamoja na ubunifu wa safu ya kiungo. Slovan inaweza kuchagua kujilinda kwa wingi na kutafuta mashambulizi ya kushtukiza, kwani kuacha nafasi nyingi nyuma dhidi ya PSG kunaweza kuwa hatari. Kwa hiyo, vita ya kwanza itakuwa kati ya uwezo wa PSG kuvunja ulinzi wa Slovan na nidhamu ya wageni katika kuzuia mashambulizi ya wenyeji.
Kwa ujumla, PSG inaonekana kuwa na nafasi kubwa zaidi ya kushinda kutokana na ubora wa kikosi, uzoefu wa Champions League na faida ya kucheza nyumbani. Hata hivyo, changamoto yao kubwa ni kutoruhusu presha ya matokeo ya ligi kuathiri mchezo huu.