Tanzanite Queens vs Canada U20
Michezo Bongo

Tanzanite Queens Kuivaa Canada: Vita ya Pointi 3 na Nafasi ya 16 Bora Kombe la Dunia U20

Vardo September 9, 2026 9:42 am

Baada ya kupata matokeo yasiyoridhisha katika mechi mbili za kwanza za Kundi B kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Wanawake chini ya umri wa miaka 20 (Poland 2026), Timu ya Taifa ya Tanzania (Tanzanite Queens) sasa inaelekeza macho yote kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Canada. Mchezo huo wa maamuzi utapigwa Septemba 11, 2026, kuanzia saa 12:00 jioni.

Tanzania inalazimika kusaka ushindi na pointi tatu muhimu ili kujiwekea matumaini ya kufuzu hatua ya 16 bora. Hii inafuatia vipigo viwili mfululizo—kwanza ikipoteza 4-1 dhidi ya Brazil kisha kukubali kichapo cha 5-1 dhidi ya Uingereza.

Katika mchezo dhidi ya Uingereza, mabao ya wapinzani yalifungwa na Rachel Maltby aliyepachika hat-trick, huku Princess Ademiluyi na Jessie Gale wakihitimisha ushindi huo. Bao la kufutia machozi la Tanzania lilifungwa na mshambuliaji Jamila Rajabu, akimalizia juhudi binafsi za mlinzi wa pembeni Diana Mnally aliyekokota mpira kutokea nyuma.

Msimamo wa Kundi B

Timu Mechi Pointi
Brazil 🇧🇷 2 6
Uingereza 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁢󠁥n🇬 2 4
Canada 🇨🇦 2 1
Tanzania 🇹🇿 2 0

Hesabu za Tanzanite Queens Kufuzu 16 Bora

Licha ya kuwa mkiani bila pointi, safari ya Tanzanite Queens nchini Poland bado haijafika kikomo. Mfumo wa mashindano ya FIFA U-20 unapanga kuwa timu mbili za juu kutoka kila kundi pamoja na timu nne bora zitakazomaliza katika nafasi ya tatu (best third-placed teams) zinasonga mbele hadi hatua ya 16 bora.

Ili kuandika historia katika ushiriki wao wa kwanza kabisa wa Kombe la Dunia, Tanzanite Queens inahitaji ushindi mnono dhidi ya Canada ili kufikisha pointi 3 na kuboresha tofauti ya mabao. Ushindi huo utaziweka pazuri dada zetu kuingia kwenye mchujo wa timu bora za nafasi ya tatu.

Nyota 4 wa Tanzanite Queens Watakaojiuza Kombe la Dunia U-20 Ukweli Kuhusu Rekodi za Mabondia Tanzania: Hassan Mwakinyo na Fadhili Majiha Wanafundisha Nini?