Kombe la Dunia la Wanawake U-20
Habari za michezo

Nyota 4 wa Tanzanite Queens Watakaojiuza Kombe la Dunia U-20

Vardo September 9, 2026 9:36 am

Tanzania haikuanza vizuri safari yake katika mechi ya kwanza ya Kombe la Dunia la Wanawake U-20 baada ya kukubali kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya miamba Brazil. Hata hivyo, ndani ya matokeo hayo mabaya, kuna mwanga wa matumaini kutokana na kiwango kilichoonyeshwa na baadhi ya wachezaji wa Tanzanite Queens.

Mashindano makubwa kama haya hayatazamwi na mashabiki pekee; makocha, mawakala na maskauti wa klabu mbalimbali duniani hufuatilia kwa karibu vipaji vipya. Kwa wachezaji vijana, dakika chache za kuonyesha uwezo uwanjani zinaweza kuwa mwanzo wa hatua kubwa kwenye taaluma yao ya soka.

Tazama wachezaji wanne walioonyesha cheche na wanaoweza kumpata mchumba wa soka la kulipwa:

  • Winfrida Gerald: Winga huyo machachari wa JKT Queens ndiye aliyeifungia Tanzania bao la kufutia machozi dhidi ya Brazil kwa mkwaju wa penalti. Zaidi ya bao hilo, Winfrida alikuwa nguzo muhimu iliyoiwezesha Tanzanite kufuzu michuano hii baada ya kufanya kweli dhidi ya Cameroon.

  • Mary Siyame: Kiungo mshambuliaji wa Fountain Gate Princess (anayekipiga Simba Queens kwa mkopo), ameonyesha uwezo mkubwa wa kumiliki mpira na kucheza maeneo tofauti ya katikati na mbele.

  • Jamila Rajabu: Mshambuliaji huyo kinda wa JKT Queens na kikosi cha Twiga Stars alionyesha uwezo mkubwa wa kuwatoka mabeki na kuingia eneo la hatari la mpinzani, silaha inayomfanya kuwa hatari wakati wote.

  • Ester Maseke: Beki wa kati wa JKT Queens alisimama imara. Licha ya mashambulizi mfululizo kutoka Brazil, Maseke alifanikiwa kuondoa hatari kadhaa na kushinda mipira mitatu ya juu ya hatari.

Kiwango kilichoonyeshwa na nyota hawa kinatoa picha kuwa, hata kama timu haitafika mbali, wana nafasi kubwa ya kujiuzia soko la kimataifa kupitia michuano hii.

Ibenge Asifu Simba, Yanga na Singida BS Michuano ya CAF Tanzanite Queens Kuivaa Canada: Vita ya Pointi 3 na Nafasi ya 16 Bora Kombe la Dunia U20