Adeyum Saleh Mbuni FC
Michezo Bongo

Adeyum Saleh Afunguka Sababu za Kujiunga na Mbuni FC, Aweka Mipango Mizito

Vardo September 20, 2026 4:31 pm

BEKI mpya wa kushoto wa Mbuni FC ya jijini Arusha, Adeyum Saleh, ameweka wazi sababu za kufikia uamuzi wa kujiunga na kikosi hicho kwa ajili ya msimu wa 2026/2027, huku akisisitiza kuwa lengo lake kuu ni kutafuta changamoto mpya baada ya kuachana na Bigman FC ya jijini Tanga.

Akizungumza na chombo cha habari, nyota huyo aliyewahi kuzichezea timu mbalimbali za Ligi Kuu zikiwemo Yanga SC, Coastal Union, Stand United, Kagera Sugar na Dodoma Jiji, alisema kuwa licha ya ugeni wake ndani ya Mbuni FC, ana amani tele na anaamini uzoefu alionao utasaidia kwa kiasi kikubwa kutimiza malengo ya timu hiyo.

“Hatujaanza vizuri msimu huu, lakini bado tuna nafasi kubwa ya kufanya vizuri mbeleni. Ligi imekuwa ngumu kutokana na ushindani wa timu zote, lakini nitapambana kwa ushirikiano na wachezaji wenzangu ili tuweze kufikia malengo,” alisema Adeyum.

Kiu ya Kufunga Mabao Zaidi Msimu Huu

Mbali na majukumu yake ya kukaba, beki huyo wa kushoto ameeleza kuwa msimu huu wa 2026/2027 ana kiu ya kufunga mabao mengi zaidi kila atakapopata fursa, kama alivyofanya msimu uliopita akiwa na Bigman FC.

Msimu wa 2025/2026, Adeyum alikuwa mchezaji wa pili kwa ufungaji ndani ya kikosi cha Bigman FC baada ya kutikisa nyavu mara 5, akitanguliwa na mshambuliaji Raia wa Nigeria, Collins Kelvin Nwobodo, aliyefunga mabao 6.

Simba SC Kuhamishia Kambi Afrika Kusini Kuitengeneza Yanga SC Kariakoo Derby Juma Masoud Afunguka Alivyochelewa Songea United, Aomba Muda Aunde Kikosi cha Maangamizi