Kambi ya Simba Afrika Kusini
Simba SC

Kambi ya Simba Afrika Kusini: Siri ya Hoteli ya Mamilioni na Wachezaji Watakaokosekana!

Vardo September 22, 2026 12:30 pm

Klabu ya Simba SC imepanga kutumia vyema mapumziko ya Ligi Kuu ya NBC kwa kuweka kambi kabambe nchini Afrika Kusini, lengo likiwa ni kukiweka kikosi hicho kwenye hali nzuri ya ushindani kabla ya kurejea kwenye michuano ya ndani na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amethibitisha kuwa kambi hiyo itafanyika katika mji wa Polokwane, Jimbo la Limpopo.

“Tunakwenda katika mji wa Polokwane, Jimbo la Limpopo… tunakwenda kuchimba huko kwa ajili ya kufanya maandalizi makubwa kabambe kuelekea Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika,” alisema Ahmed Ally.


Hoteli ya Kifahari na Miundombinu ya Kimataifa

Ingawa uongozi wa Simba haujataja rasmi jina la hoteli watakayofikia, taarifa za ndani zinaeleza kuwa Wekundu wa Msimbazi huenda wakajichimbia katika hoteli ya kifahari ya Protea Hotel Polokwane Ranch Resort, iliyopo takribani kilomita 25 kusini mwa mji wa Polokwane.

Eneo hilo si sehemu ya malazi pekee, bali lina miundombinu ya kisasa inayokidhi viwango vya kimataifa kwa timu kubwa za soka:

  • Uwanja wa Mpira wa Ukubwa Kamili: Pamoja na viwanja viwili vya mazoezi vya matumizi mbalimbali.

  • High Performance Centre: Maalum kwa ajili ya mazoezi ya nguvu na programu za kurejesha uwezo wa mwili (recovery).

  • Mazingira ya High-Altitude: Ipo mita 1,300 kutoka usawa wa bahari, mazingira yanayosaidia kuongeza stamina ya wachezaji.

  • Faragha na Usalama: Eneo hilo limewahi kutumiwa na klabu kubwa kama Mamelodi Sundowns, Kaizer Chiefs, Orlando Pirates, pamoja na timu za kimataifa kama Manchester City, Tottenham Hotspur na Timu ya Taifa ya Senegal.


Ratiba ya Safari na Mipango ya Kocha Steve Barker

Kocha Mkuu wa Simba, Steve Barker, tayari yupo nchini Afrika Kusini akishirikiana na benchi lake la ufundi kuandaa mazingira na programu maalum kabla ya kikosi kuwasili.

Wachezaji kadhaa wa kimataifa akiwemo Rushein De Reuck, Ibraheem Jabaar, Neo Gift Maema na Kalesto Makgalwa tayari wamewasili nchini humo. Baki ya kikosi kinachotokea Tanzania kinatarajiwa kuondoka Septemba 24 na kuungana na wenzao mkoani Johannesburg kabla ya kuelekea Polokwane kuanza kazi rasmi.


Orodha ya Wachezaji Watakaokosekana Kambini

Hata hivyo, Simba itaingia kambini ikiwa haina baadhi ya nyota wake muhimu kutokana na kukabiliwa na majukumu ya timu zao za taifa:

  1. Wachezaji wa Kimataifa:

    • Enno Loemba (Congo-Brazzaville)

    • Mahamadou Kasali

  2. Nyota wa Watanzania (Majukumu ya Kimataifa):

    • Morris Abraham

    • Yusuf Kagoma

    • Vedastus Masinde

    • Antony Mligo

    • Nathaniel Chilambo

Mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi mnasubiri kwa hamu kuona matunda ya kambi hii pindi ligi na michuano ya kimataifa itakaporejea!

Lucas Kikoti Anena Mzito: Aipongeza Safu ya Yanga, Amchagua Maxi Nzengeli Ahmed Ally Afichua Siri ya Simba SC Kuzisambaratisha ‘Timu Korofi’ Ligi Kuu