Rushine De Reuck Simba SC
Simba SC

Hali Ilikuwa Mbaya! Rushine De Reuck Avunja Ukimya Ndani ya Simba SC

Vardo September 23, 2026 11:39 am

Beki wa zamani wa Mamelodi Sundowns na timu ya taifa ya Afrika Kusini, Rushine De Reuck, amefunguka mazito kuhusu maisha yake mapya ndani ya Simba SC, akikiri kuwa alitua nchini akiwa amevunjika moyo kabisa na kujawa na mashaka makubwa juu ya kiwango chake.

De Reuck ameweka wazi kuwa kukosekana kwa nafasi ya kucheza mara kwa mara nchini kwao kulimfanya aanze kujitilia shaka na kujiuliza kama bado anao uwezo wa kucheza soka la ushindani la kulipwa. Hata hivyo, hali hiyo ilianza kubadilika mara tu alipotua katika ardhi ya Tanzania kujiunga na wekundu wa Msimbazi, Simba SC.

Akizungumzia mabadiliko hayo, beki huyo alieleza kuwa Kocha Fadlu Davids alikuwa mtu wake wa kwanza wa karibu aliyempa mwanga wa matumaini.

“Nilikuja Tanzania nikiwa na hofu kubwa. Nilikuwa nimekaa muda bila kucheza na nikaanza kujiuliza kama bado ninaweza kucheza soka la kulipwa,” alisema De Reuck.

Licha ya mashaka hayo, mapokezi mazuri kutoka kwa uongozi, benchi la ufundi, na mashabiki wa Simba SC yalimrudishia hali yake ya kujiamini hatua kwa hatua. Kwa sasa, De Reuck anasema Tanzania si tu kituo cha kazi, bali ni sehemu iliyomrudishia upendo, tabasamu, na furaha ya kucheza mpira iliyokuwa imepotea.

Bakari Msimu: Benchi la Simba Limesimama Kama Darasa Langu Ibraheem Jabaar Afunguka: Kadi Nyekundu Pamba Jiji ni Funzo Kubwa