Ibraheem Jabaar Simba
Simba SC

Ibraheem Jabaar Afunguka: Kadi Nyekundu Pamba Jiji ni Funzo Kubwa

Vardo September 23, 2026 11:45 am

Kiungo mpya wa Simba SC, Ibraheem Jabaar, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto kubwa aliyokutana nayo tangu atue Tanzania, akitaja kadi nyekundu aliyoipata dhidi ya Pamba Jiji kuwa funzo kubwa ambalo hataki kulirudia maishani mwake ya soka.

Jabaar, raia wa Nigeria aliyetua Msimbazi akitokea Stellenbosch FC ya Afrika Kusini, amekuwa miongoni mwa wachezaji wapya walioonyesha kiwango bora chini ya kocha Steve Barker. Hata hivyo, mwanzo wake uligubikwa na utata Agosti 19 alipolimishwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Pamba Jiji kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo huyo mwenye umri wa miaka 23 alikiri makosa yake na kusema kuwa ni sehemu ya hisia za mchezo ambazo alishindwa kuzizuia kwa muda huo.

“Nilijiambia ‘come on, Ibraheem unawezaje kufanya hivi?’ Wakati mwingine unashindwa kujizuia kwa sababu damu inakuwa imechemka. Lakini najifunza kutokana na makosa yangu, na nina uhakika haitatokea tena,” alisema Jabaar.

Kuelekea Ligi ya Mabingwa na Dabi

Licha ya kuanza kwa changamoto hiyo, Jabaar anaamini kikosi cha Simba kina ubora wa kutosha kufanya makubwa msimu huu, hasa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Ligi Kuu Bara. Amewataja wachezaji wenzako kama Clatous Chama na wengine kuwa nguzo muhimu za kuifikisha timu mafanikio.

Kuhusu hali ya hewa ya Tanzania, staa huyo alidokeza kuwa haijawa tatizo kwake kwa sababu inafanana kwa kiasi kikubwa na kwao Nigeria, jambo lililomfanya azowee haraka.

Huku lengo kuu likiwa ni kurejesha taji la ubingwa Msimbazi, Jabaar amewatoa hofu mashabiki wa Simba na kuwaahidi kujituma kwa asilimia mia moja ili kulipa imani kubwa waliyonayo kwake.

Hali Ilikuwa Mbaya! Rushine De Reuck Avunja Ukimya Ndani ya Simba SC Ajali ya Kutisha na Supu ya Miguu ya Kuku: Siri ya Kupona ya Andros Townsend