Arda Guler: Silaha Mpya ya Real Madrid na Ukame wa Miaka 120 Waisha!
HISPANIA – Baada ya miaka kadhaa ya kusubiri na kuhangaika kupitia mrithi wa wataalamu wa zamani wa mipira ya adhabu (iliyokufa), kuibuka kwa staa kijana Arda Guler kumeifungulia Real Madrid ukurasa mpya wa mafanikio na kuwapa silaha ya kutisha kwenye eneo hilo chini ya kocha Jose Mourinho.
Kuondoka kwa mastaa wakubwa kama Cristiano Ronaldo, Gareth Bale, Sergio Ramos, na Toni Kroos kuliacha pengo kubwa la wachezaji wenye uwezo wa kutendea haki mipira ya adhabu ya moja kwa moja. Hata hivyo, Guler sasa ameonekana kuwa suluhu ya kudumu kutokana na uwezo wake wa kipekee na imani anayozidi kupewa na benchi la ufundi.
Katika mchezo dhidi ya Elche, dakika 25 tu baada ya mpira kuanza, kiungo huyo wa kimataifa wa Uturuki aliandika historia baada ya kupiga mpira safi wa adhabu uliomshinda kipa Matías Dituro na kuingia wavuni moja kwa moja, huku ukiipa Madrid ushindi na kumpa yeye mwenyewe sifa kedekede.
Bao hili limeweka ukomo rasmi kwenye ukame mrefu zaidi katika historia ya La Liga ambapo Real Madrid ilicheza mechi 120 mfululizo za ligi bila kufunga bao kutokana na mpira wa adhabu ya moja kwa moja. Mara ya mwisho kwa Los Blancos kufunga kupitia njia hiyo ilikuwa ni msimu wa 2022-23 kupitia kwa Rodrygo Goes dhidi ya Sevilla.
Akizungumzia kiwango cha staa huyo, kocha Jose Mourinho alionyesha kuridhishwa na mchango wa mchezaji huyo akisema: “Arda ni bora kwa sasa na anafanya kile kinachotakiwa uwanjani.”