Wachezaji wa Yanga timu ya taifa
Yanga SC

Yanga Yamwaga Kikosi Kizima Timu za Taifa: 15 Waitwa!

Vardo September 23, 2026 11:20 am

Klabu ya Yanga SC imetamba kwa ubora wa kikosi chake baada ya wachezaji 15 kutoka kikosi cha kwanza kuitwa kwenye vikosi mbalimbali vya timu za taifa kwa ajili ya majukumu ya kimataifa katika kipindi hiki cha mapumziko ya Ligi Kuu Bara.

Akizungumzia mafanikio haya, Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kuwa idadi hiyo kubwa ni ishara tosha ya kazi nzuri inayofanywa na uongozi pamoja na benchi la ufundi katika kujenga timu yenye wachezaji wa viwango vya juu vinavyotakiwa kimataifa.

“Tumetoa wachezaji takribani 16 kwenye ngazi mbalimbali za timu za Taifa. Wachezaji 10 wamekwenda kwenye timu za Taifa za wakubwa, huku wengine wakiwa kwenye vikosi vya vijana vya Under-20 na Under-23. Jumla ya wachezaji 15 kutoka kwenye kikosi chetu kikuu wamepata nafasi ya kuitumikia nchi zao,” alieleza Kamwe.

Aliongeza kuwa hali hiyo inadhihirisha ushindani uliopo ndani ya klabu hiyo na ubora wa wachezaji wao katika mashindano ya ndani na kimataifa.

Mpango Kazi Wakati wa Mapumziko

Wakati wachezaji hao wakiwa kwenye majukumu ya kitaifa, kikosi kilichosalia klabuni kimepewa mapumziko ya siku nane kabla ya kurejea rasmi kambini Avic Town, Geita.

Baada ya hapo, wachezaji wataanza maandalizi ya awali kwa ajili ya kuendelea kwa Ligi Kuu Bara na michuano mikubwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika, wakisubiri kuungana na wenzao mara baada ya kumaliza majukumu ya timu za taifa.

Takwimu za Yanga Zashtua Ligi Kuu: Ubabe wa Kamwe Waacha Gumzo! Bakari Msimu: Benchi la Simba Limesimama Kama Darasa Langu