Siri Yafichuka! Kim Kardashian na Lewis Hamilton Wazama Kwenye Mapenzi Baada ya Miaka 12
Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian, kwa sasa anagonga vichwa vya habari duniani kote kufuatia kuthibitika kwa uhusiano wake wa kimapenzi na staa wa mchezo wa mbio za magari wa Formula 1, Lewis Hamilton, kutokea Uingereza.
Licha ya Kim kumpenda Hamilton kwa muda mrefu, ilimbidi dereva huyo mashuhuri kusubiri kwa takribani miaka 12 kabla ya kuanzisha rasmi uhusiano wa kimapenzi na mwanamitindo huyo.
Historia ya Mapenzi ya Kim Kardashian
Kim, ambaye ni mtangazaji na mshiriki wa kipindi mashuhuri cha Keeping Up with the Kardashians, amewahi kuhusishwa na wanaume kadhaa huko nyuma na kufunga ndoa mara tatu:
-
Damon Thomas: Aliolewa naye akiwa na umri wa miaka 19 (mwaka 2000). Ndoa yao ildumu kwa miaka mitatu kabla ya kutengana mwaka 2003.
-
Kris Humphries: Mchezaji huyu wa zamani wa NBA (New Jersey Nets) alimuoa Kim mnamo Agosti 2011, lakini ndoa yao ilivunjika baada ya siku 72 tu.
-
Kanye West (Ye): Walifunga ndoa Florence, Italia mnamo Mei 2014 na kufanikiwa kupata watoto wanne, kabla ya kupeana talaka rasmi mwaka 2022.
Tangu kuachana kwake na Kanye West, Kim hakuwahi kuthibitisha wazi uhusiano wowote wa kimapenzi hadi alipofanya hivyo sasa akiwa na Lewis Hamilton.
Kutoka Kutamani Kuwa Single Hadi Kuangukia Kwenye Mahaba
Mnamo Novemba 2025, kupitia kipindi chake cha Keeping Up With The Kardashians, Kim alieleza hamu yake ya kuendelea kuwa bila mpenzi (single):
“Unapokaa muda mrefu ukiwa single, unazidi kuzoea, na mawadonzi ya kuwa na mtu wa karibu yanapungua na hata kukosa mvuto,” alisema Kim.
Kauli hii ilikuja baada ya mwigizaji Sarah Paulson, aliyetokea naye kwenye tamthilia ya All’s Fair (2025), kumshauri Kim kuweka kando ulinzi mkali wa moyo wake na kumpa nafasi mwanamume mwingine.
Wakati huo, Hamilton alikuwa akifuatilia hali hiyo kwa karibu, kwani tetesi za wawili hao kuwa pamoja zilianza kusambaa miezi miwili baadaye.
Urafiki wa Miaka 10 Uliogeuka Kuwa Mapenzi Mazito
Kim Kardashian na Lewis Hamilton wamekuwa marafiki kwa zaidi ya miaka 10, tangu Kim akiwa kwenye ndoa na Kanye West.
-
2014 (GQ Men of the Year): Kim alisalimiana na Hamilton kwa kumbusu shavuni kama ishara ya urafiki wa kawaida.
-
2021 & 2023: Walizidi kuonekana pamoja kwenye matukio makubwa kama WSJ. Magazine Innovator 2021 na shoo ya Pharrell Williams mwaka 2023.
-
Februari 2, 2026: Mtandao wa TMZ ulinasa video ya wawili hao wakiwasili kwenye hoteli moja jijini Paris, Ufaransa wakitokea Uingereza kwa ndege binafsi (Private Jet).
Ilidaiwa kuwa safari hiyo ya Paris ilikuwa na lengo la kujadili namna ya kuuweka uhusiano wawe wazi kwa umma bila kuathiri heshima au faragha zao.
Uthibitisho Rasmi wa Uhusiano Waao
Wiki moja baadaye, walionekana pamoja katika tukio kubwa la Super Bowl LX wakiwa wamekaa kwenye chumba maalumu (VIP Box). Siku iliyofuata, Hamilton alionekana kwenye video iliyochapishwa na Kim kwenye ukurasa wake wa Instagram—jambo lililothibitisha rasmi kuwa ni wapenzi.
Chanzo cha karibu kilichozungumza na jarida la People kilieleza:
“Hamilton ni mwanamume ambaye amemvutia Kim kwa dhati kwa muda mrefu. Anamfanya Kim ajisikie salama na anafurahia sana kutumia muda wake pamoja naye.”
Mwezi Januari 2026, kwenye podcast ya dada yake, Khloe in Wonder Land, Kim alitaja sifa za mwanamume anayemtaka:
“Awe mtu mwenye maadili na misingi mizuri, mtulivu, anayeaminika na anayekubali kuwajibika. Hicho ndicho kipaumbele changu namba moja.”
Ni wazi kuwa ndoto ya Kim Kardashian imetimia mikononi mwa Lewis Hamilton, kwani kwa sasa wawili hao wanaonekana huru kufurahia maisha na kuchapisha picha za pamoja mitandaoni.