Clara Luvanga Washington Spirit
Michezo Bongo

Clara Luvanga Aweka Historia Marekani, Ashinda Tuzo ya Bao Bora NWSL

Vardo October 8, 2026 6:48 pm

MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Clara Luvanga, anaendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi nchini Marekani baada ya bao lake alilofunga wiki iliyopita kutangazwa kuwa Bao Bora la Wiki katika Ligi Kuu ya Wanawake nchini humo (NWSL).

Nyota huyo anayecheza klabu ya Washington Spirit aliingia kwenye kinyang’anyiro hicho kufuatia kiwango chake bora kwenye mchezo dhidi ya Houston Dash uliopigwa Oktoba 5, 2026.

Katika mchezo huo wa kusisimua ambapo Washington Spirit iliibuka na ushindi wa mabao 3-2, Clara aliingia kipindi cha pili na kucheza dakika 25 pekee, lakini alihitaji dakika ya 84 kufunga bao la ushindi lililowapa pointi tatu muhimu.

Awatupa Nje Nyota Wengine wa NWSL

Bao hilo la kiwango cha juu lilimwezesha kuingia kwenye kinyang’anyiro cha kuwania tuzo hiyo, ambapo alikuwa akichuana na wachezaji wengine wakali wa ligi hiyo.

Katika kura zilizopigwa na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii, Clara aliwashinda wenzake waliokuwa wakewania tuzo hiyo ambao ni:

  • Miljana Ivanovic (Houston Dash)

  • Lia Godfrey (San Diego Wave FC)

  • Brecken Mozingo (Utah Royals FC)

Mwanzo Mzuri Katika Soka la Marekani

Mchezo huo ulikuwa wa pili kwa Clara tangu ajiunge na Washington Spirit Septemba 9, 2026, akitokea Al Nassr ya Saudi Arabia kwa mkataba wa miaka minne—uhamisho ulioweka rekodi kubwa.

Alianza kucheza mechi yake ya kwanza Septemba 26, 2026, dhidi ya Angel City FC ambapo aliingia kutokea benchi na kucheza dakika 24 kwenye mchezo ambao timu yake ilipoteza kwa bao 1-0.

Mafanikio haya yanaendeleza muundo wake mzuri wa ufungaji aliotoka nao Al Nassr, ambako alikuwa mfungaji bora wa ligi msimu uliopita baada ya kupachika mabao 24 kambani.

Clara Azungumza Baada ya Ushindi

Akizungumza kuhusu mafanikio hayo, Clara alisema:

“Kwangu ni kitu kizuri kuanza msimu na bao kwenye ligi ngumu kama ya Marekani ambayo ina wachezaji wengi wazuri na wenye ushindani mkubwa.”

Clara Luvanga anaingia kwenye vitabu vya kumbukumbu kama mchezaji wa kwanza mwanamke kutoka Tanzania kucheza katika Ligi Kuu ya Wanawake nchini Marekani (NWSL).

Télécharger 1xbet APK – méthodes de paiement et guide d’installation en France