Kombe la EPL Tanzania
Michezo

Guinness Kulizungusha Kombe La EPL Dar

Vardo October 9, 2026 2:51 pm

Jiji la Dar es Salaam leo limefurika msisimko mkubwa baada ya kupokea moja ya makombe yenye mashabiki wengi zaidi wa soka duniani—taji la Ligi Kuu Uingereza (EPL).

Kupitia udhamini wa Guinness, kombe hilo rasmi la EPL limewasili nchini Tanzania na linafanya ziara katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ili kuwapa mashabiki fursa ya kushuhudia historia hiyo karibu zaidi.

Ratiba ya Ziara na Matukio:

  • Leo Jioni (The Superdome – Masaki): Baada ya kumaliza ziara ya mitaani, shughuli rasmi na usiku wa burudani utaendelea katika ukumbi wa The Superdome uliopo Masaki.

  • Kesho (KMC Complex – Mwenge): Mashabiki na wapenzi wa soka watakutana katika uwanja wa KMC Mwenge kwa ajili ya siku maalum ya soka, burudani, pamoja na kupiga picha na kutengeneza kumbukumbu za maisha na ndoo hiyo ya EPL.

Usikose fursa hii ya kuwa sehemu ya historia ya soka nchini!

Kombe la EPL Latuwa Tanzania: TFF na SBL Waeleza Fursa Nje ya Uwanja Steve Barker Aweka Wazi Mbinu 3 Za Kuichapa Yanga Dabi ya Kariakoo