Hemed Morocco Atema Nyongo: Kuahirishwa kwa Mechi ya Yanga na TRA United Kumevuruga Mipango Yangu!
Kocha Mkuu wa TRA United, Hemed Suleiman ‘Morocco’, amefunguka na kueleza kusikitishwa kwake na uamuzi wa kuahirishwa kwa mchezo wao wa Ligi Kuu dhidi ya Yanga uliokuwa umepangwa kuchezwa leo, akidai hatua hiyo imetibua moja kwa moja mipango ya benchi la ufundi.
Mchezo huo uliokuwa uchezwe kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini Arusha, umesogezwa mbele hadi tarehe Oktoba 24, 2026. Hatua hii imechukuliwa ili kuipa nafasi Yanga kujiandaa vizuri na pambano lao muhimu la Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya CFFA FC ya Madagascar.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Morocco alieleza kuwa kukaa wiki mbili nzima bila kupata mchezo wa ushindani ni pigo kubwa kwa timu yake, hasa ikizingatiwa kuwa walikuwa na kiu ya kusahihisha makosa baada ya kupokea kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Namungo FC mnamo Oktoba 8, 2026.
“Tunaiheshimu Yanga na majukumu yao ya kimataifa, lakini kucheza leo kungetuongezea kasi. Kutoka Oktoba 8 hadi 24 ni wiki mbili kamili bila ushindani; hii itatuathiri sana kwa sababu wenzetu wataendelea kuwa na mwendelezo wa mechi na programu za ushindani,” alisema Morocco.