Azam FC

Kikosi cha Azam FC Chaondoka Kwenda Misri Kuwakabili Zed FC Kombe la Shirikisho

Vardo October 13, 2026 8:02 am

Kikosi cha timu ya wananchi wa Chamazi, Azam FC, kimewasili rasmi nchini Misri baada ya kuondoka leo Jumatatu asubuhi kuelekea jijini Cairo kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Zed FC.

Mchezo huo wa kusisimua utapigwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo siku ya Ijumaa, Oktoba 16, 2026, ukianza majira ya saa 2:00 usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Azam FC Kuingia na Rekodi Nzuri

Wawakilishi hawa wa Tanzania wanatua Misri wakiwa na kumbukumbu nzuri ya kiwango chao bora msimu uliopita wa 2025/2026, ambapo walifanikiwa kutinga hatua ya makundi na kumaliza nafasi ya tatu katika Kundi B wakiwa na pointi tisa. Walinyuma nyuma ya Maniema (pointi 12) na vinara Wydad Athletic waliokusanya pointi 15.

Kwa upande wa Zed FC, wenyewe walitinga hatua hii baada ya kuwatupa nje ASAS ya Djibouti kwa jumla ya mabao 5-1. Walishinda 4-0 wakiwa nyumbani kabla ya kulazimishwa sare ya 1-1 ugenini.

Hali za Timu Katika Ligi za Ndani

  • Azam FC: Inaendelea vizuri kwenye Ligi Kuu, ambapo hadi sasa imecheza michezo 8, imeshinda 5, imetoka sare 2 na kupoteza mmoja pekee, huku ikishika nafasi ya tatu na pointi zake 17.

  • Zed FC: Kwenye Ligi Kuu ya Misri, wamecheza mechi 5, wakishinda mbili, sare moja na kupoteza mara mbili, na wanashika nafasi ya 11 wakiwa na pointi saba.

Hemed Morocco Atema Nyongo: Kuahirishwa kwa Mechi ya Yanga na TRA United Kumevuruga Mipango Yangu! Mambo Yapo Meridianbet na UEFA Leo