Ligi Daraja la Kwanza Zanzibar
Michezo Bongo

Ligi Daraja la Kwanza Zanzibar: Taifa Jang’ombe Yakingia Kifua Kundi A, Rangers Bulls Yapata Taabu

Vardo October 18, 2026 8:31 pm

Ligi Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja msimu wa 2026-2027 imezidi kuchanja mgongo huku ushindani ukiwa mkubwa, huku timu nne zikijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kushindwa kupata ushindi wowote tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Kati ya timu hizo, tatu zinatoka Kundi A ambazo ni Bweleo Warriors, Kikungwi Stars, na Malindi, wakati Rangers Bulls ikiwa ndiyo timu pekee kutoka Kundi B ambayo haijapata ushindi wala pointi hadi sasa.

Hali Ilivyo Katika Kundi A

Kundi hili linaongozwa kwa kishindo na Taifa Jang’ombe, yenye pointi 12 baada ya kushinda mechi zake zote nne ilizocheza, ikiwa haijapoteza wala kutoa sare.

Nafasi ya pili inashikilia na New King yenye pointi 7 kutokana na mechi tatu (ushindi mbili na sare moja), zikiwa ni alama tano nyuma ya vinara. Negro United inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 5, sawa na Mundu iliyo nafasi ya nne. Timu ya Malindi, iliyoshuka daraja msimu uliopita, inaburuza mkia katika kundi hili lenye jumla ya timu tisa.

Mapambano Kundi B

Kwenye Kundi B, usunguliaji unaongozwa na Kundemba yenye pointi 9, ikiwa na pointi sawa na Kitope United iliyo nafasi ya pili. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Paje Star yenye pointi sita, wakati New City inakamata nafasi ya nne ikiwa na pointi tano.

Hata hivyo, Rangers Bulls inaendelea kusota baada ya kuwa timu pekee kwenye kundi hilo isiyovuna alama hata moja baada ya kupoteza michezo yake yote mitatu ya kwanza.

Terence Crawford Awa Mlezi Rasmi wa Ligi ya Ngumi Dunda Tanzania! Kocha wa Alliance Girls Afichua Siri ya Timu Kabla ya Ligi Kuu