Simba SC Ligi ya Mabingwa Afrika
Simba SC

Steve Barker Atangaza Lengo Kuu Simba SC Ligi ya Mabingwa Afrika

Vardo October 18, 2026 8:36 am

Kocha mkuu wa Simba SC, Steve Barker, ameweka wazi kuwa kikosi chake kimefanya maandalizi ya kina kwa ajili ya mchezo ujao dhidi ya 15 de Agosto ya Equatorial Guinea katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, akisisitiza kuwa kipaumbele chao kikubwa ni kutinga hatua ya makundi.

Akizungumzia maandalizi hayo, Barker ameeleza kuwa Simba ina malengo makubwa msimu huu, na kutambua umuhimu wa kuanza mashindano hayo kwa ushindi na matokeo mazuri ili kujenga msingi imara wa safari yao barani Afrika.

Kikosi hicho kilikaa kambini kwa takribani miezi miwili, kikiwa kimefanyia mazoezi yake huko Kigali, Rwanda, na Polokwane, Afrika Kusini. Kocha huyo alieleza kuwa programu hizo zimewasaidia kujenga ushindani wa hali ya juu, huku benchi la ufundi likiendelea kufanya marekebisho madogo madogo ya mwisho ili kuhakikisha wachezaji wapo katika ubora wao kamili.

“Pamoja na maendeleo yaliyofikiwa, Simba bado ina nafasi ya kuboresha zaidi mchezo wake, kipaumbele kikiwa ni kuhakikisha tunavuka kizingiti cha 15 de Agosto na kuendelea na harakati za kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Barker.

Simba SC Yamtangaza Rasmi 15 de Agosto: Mchezo Kuchezwa Bila Mashabiki! Ally Kamwe: Yanga SC Haizuiliki, Malengo ni Ubingwa Afrika!