Ali Kamwe Yanga
Yanga SC

Yanga SC Ni Mfano wa Kuigwa Afrika – Ali Kamwe Atuma Ujumbe Mzito

Vardo October 24, 2026 12:16 pm

Msemaji wa Yanga, Ali Kamwe, amezitaka klabu za soka nchini Tanzania kuacha kuridhika na mafanikio ya muda mfupi na badala yake zifunze kutoka Yanga namna ya kujenga timu shindani na kudumisha mafanikio katika mashindano ya kimataifa.

Akizungumza hivi karibuni, Kamwe alieleza kuwa kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa misimu 4 mfululizo ni ishara tosha ya weledi, utulivu, na uwezo mkubwa uliojengwa ndani ya klabu hiyo, jambo ambalo linapaswa kuigwa na timu nyingine zinazotaka kufika mbali.

“Uliza timu yako ni wapi imefanya hivyo, ni wapi imecheza hatua ya makundi ya CAF Champions League mara nne mfululizo. Kama jibu ni hapana, basi weka mkono hapa, wapigie salute Yanga,” alisema Kamwe kwa kujiamini.

Kusubiri Droo ya Makundi Oktoba 28

Kuhusu hatua inayofuata, Kamwe alithibitisha kuwa klabu hiyo ipo tayari na inasubiri droo rasmi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa Oktoba 28, kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Baada ya hapo, uongozi utatoa mwongozo kamili kwa wanachama na mashabiki kuhusu maandalizi ya kikosi hicho.

Lengo Lilibadilika: Kutoka Robo Fainali hadi Ubingwa wa Afrika

Katika hatua nyingine, Kamwe alifichua kuwa awali uongozi ulikuwa na lengo la kufika hatua ya robo fainali pekee. Hata hivyo, ujio wa kocha mwenye uzoefu mkubwa, Gamondi, ulibadilisha kabisa mtazamo na kuongeza malengo ya kupigania taji kuu la Afrika.

Kocha huyo aliwaaminisha viongozi kuwa kikosi kilichopo kina uwezo kamili wa kubeba ubingwa, jambo lililoongeza ari na imani kubwa ndani ya klabu hiyo kuelekea michuano hii mikubwa barani Afrika.

Simba SC Yamtaka 15 de Agosto: Kazi Iendelee Ligi ya Mabingwa! Anuary Jabir Atishaa! Kinara wa Mabao Ligi Kuu Atuma Onyo Kali kwa Simba na Yanga