Bernard Kamungo
Michezo Bongo

Kipute cha MLS: Bernard Kamungo Avunja Rekodi ya Siku 408 Bila Goli!

Vardo October 26, 2026 8:37 am

LEO Oktoba 26, 2026, mshambuliaji matata wa Tanzania anayekipiga kikosi cha FC Dallas nchini Marekani, Bernard Kamungo, anafikisha siku 408 kamili bila kufunga bao kwenye ligi hiyo ngumu ya MLS.

Kamungo, ambaye huu ni msimu wake wa nne kuitumikia timu hiyo tangu ajiunge nayo mwaka 2023 akitokea North Texas SC alikocheza mechi nne tu, amekuwa kwenye wakati mgumu wa kusaka utupiaji tangu alipofunga mara ya mwisho Septemba 13, 2025. Kwenye msimu wa 2025/26, staa huyo alipachika mabao mawili pekee katika mechi 30, na tangu wakati huo hajatinga kambani zaidi ya kutoa asisti mbili za msimu huu.

Safari na Historia ya Kamungo MLS Nyota huyo aliyezaliwa Kasulu, Tanzania, Januari 1, 2002, alianza kung’ara mapema akiwa na kikosi cha pili cha North Texas SC mwaka 2022 alipofunga mabao 16 na kutoa asisti tano katika mechi 25, jambo lililompa tiketi ya kupandishwa kikosi cha kwanza.

Tangu aanze kucheza MLS, Kamungo alichora historia ya kukumbukwa ikiwemo bao lake la kwanza la ushindi alilofunga Aprili 15, 2023, dhidi ya Real Salt Lake dakika ya 88 akitokea benchi. Hata hivyo, ukame huu wa sasa unampa changamoto mpya ya kupambana kurudisha makali yake uwanjani.

Rekodi Mpya! Azam FC Yaandika Historia Kombe la Shirikisho Afrika