Simba SC Hatua ya Makundi CAF
Simba SC

Simba SC Yaanza Mipango Hatua ya Makundi CAF, Uwanja wa Uhuru Kutumika?

Vardo November 5, 2026 9:17 am

Klabu ya Simba SC imeanza rasmi maandalizi kabambe ya kuelekea michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) msimu wa 2026/27, huku uongozi ukipambana kuhakikisha masuala ya miundombinu ya viwanja yanakaa sawa mapema.

Licha ya kikosi hicho kuwa mapumzikoni katika mwezi huu wa Novemba, Maafisa wa Simba tayari wameanza kazi ya nyuma ya pazia kuelekea pambano lao la kwanza dhidi ya miamba ya Afrika Kusini, Orlando Pirates, pamoja na mechi nyingine zinazofuata katika kundi hilo.

Mazungumzo ya Uwanja wa Uhuru na CAF

Akitolea ufafanuzi hatua hiyo, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ameeleza kuwa uongozi upo kwenye mazungumzo ya kina na wamiliki wa Uwanja wa Uhuru pamoja na Serikali.

Lengo kuu la mazungumzo hayo ni kufanya maboresho yanayotakiwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili uwanja huo upate idhini ya kutumika kwenye michezo ya kimataifa kama mbadala.

“Tunatarajia kupata majibu kamili kuhusu uwezekano wa kukamilika kwa marekebisho hayo kabla ya mchezo wetu wa kwanza wa nyumbani dhidi ya Orlando Pirates,” alisema Ahmed Ally.

Uwanja wa Mkapa Kubaki Chaguo la Kwanza

Pamoja na jitihada hizo kwenye Uwanja wa Uhuru, Ahmed amesisitiza kuwa dhamira kuu ya Simba SC ni kuendelea kutumia Uwanja wa Benjamin Mkapa kama uwanja wao mkuu wa nyumbani.

Mipango inayofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru ni sehemu ya mkakati wa klabu hiyo kuwa na suluhisho la akiba (backup plan) ili kujikinga na changamoto zozote za miundombinu inayokidhi vigezo vya CAF.

Simba SC Yaweka Mikakati Mizito Mapumziko ya FIFA: Kambi Na Mechi za Kirafiki Kupikwa Steve Barker Kutumia Mapumziko ya FIFA Kuisuka Upya Simba SC