Yanga SC Ligi ya Mabingwa Afrika
Yanga SC

Ali Kamwe Apuuza Zamalek, MC Alger: “Tutabonda Nyumbani, Kunyonga Nje!”

Vardo November 12, 2026 12:13 pm

Afisa Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ali Kamwe, ameonyesha kujiamini kukubwa kuelekea mechi za Hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL) msimu wa 2026/27, akisisitiza kuwa hakuna timu yoyote katika Kundi B yenye uwezo wa kuzima ndoto zao za kutinga Robo Fainali.

Wananchi wamepangwa katika kundi hilo la ‘kifo’ linalojumuisha miamba ya soka kutoka Kaskazini mwa Afrika: Zamalek SC (Misri), MC Alger (Algeria), na Club Africain (Tunisia). Licha ya historia na uzoefu mkubwa wa wapinzani hao, Kamwe ameweka wazi kuwa jina au ukubwa wa timu hizo hauzitishi mbinu na maandalizi ya Yanga.

Kaulimbiu Mpya: “Kubonda Nyumbani, Kunyonga Nje”

Akizungumza kuhusu malengo ya klabu hiyo, Kamwe alisema Lengo kuu ni kumaliza katika nafasi mbili za juu ili kukata tiketi ya hatua ya Robo Fainali bila visingizio.

“Wapinzani wetu hawana chochote cha kututisha. Lengo letu ni moja tu — kuvuka hatua ya makundi na kusonga mbele hadi robo fainali. Kundi hili si gumu, na kama kutakuwa na ugumu wowote basi tutakuwa tumejiletea wenyewe,” amesema Kamwe.

Akiweka msisitizo kwenye mbinu watakayotumia, Kamwe alitaja kaulimbiu ya msimu huu: ‘Kubonda Nyumbani, Kunyonga Nje’.

“Naamini tukirekebisha baadhi ya mambo ya kiufundi yaliyokuwa changamoto, kaulimbiu yetu itaonekana kwa vitendo. Tutabonda watu hapa nyumbani Tanzania na kwenda kuwanyonga huko huko kwao. Hatuna mashaka na hilo kabisa,” aliongeza.

Sababu za Yanga Kujiamini Kundi B:

  1. Ubingwa wa Ndani na Ubora wa Ligi: Yanga inainingia ikiwa na heshima ya kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania, huku Ligi Kuu ya NBC ikiwa inashikilia nafasi ya 5 kwa ubora barani Afrika.

  2. Benchi Jipya la Ufundi: Uzoefu wa benchi la ufundi kuhusu soka la Kaskazini mwa Afrika unatarajiwa kuwa silaha kuu ya mbinu dhidi ya MC Alger, Zamalek, na Club Africain.

  3. Morali ya Wachezaji: Hali ya kujituma na morali ya kikosi ipo juu sana tayari kwa mapambano.

Kipanya Kwenye Mchezo wa Kwanza

Yanga inatarajiwa kuanza kampeni zake za Kundi B kati ya Novemba 27 na 29, 2026, ambapo itawakaribisha MC Alger katika mchezo wa ufunguzi kabla ya kusafiri kukabiliana na mechi zilizobaki za kundi hilo.

Sibusiso Makhula Afichua Siri ya Mafanikio na Umoja Ndani ya Simba SC Gamondiatoa Tamko Kali: Hatujasafiri Kwenda Nigeria Kuwa Ngazi ya Mtu!