Kikosi cha Yanga SC
Yanga SC

Habari Njema Yanga SC: Yao na Abuya Warejea Uwanjani, Pacome Apaa Ufaransa!

Vardo November 13, 2026 5:03 pm

Kikosi cha Yanga SC kimepata nguvu mpya katika maandalizi yake ya mechi zijazo baada ya nyota wake, beki Yao Kouassi na kiungo Duke Abuya, kuanza rasmi mazoezi ya pamoja na wenzao kwa mara ya kwanza tangu walipokaa nje ya uwanja kutokana na majeraha.

Akizungumza na wanahabari, Msemaji wa Yanga SC, Ali Kamwe, amethibitisha kuwa wachezaji hao wameonyesha maendeleo makubwa baada ya kukamilisha programu maalumu za kurejesha utimamu wa mwili chini ya uangalizi wa madaktari na wataalamu wa viungo wa klabu hiyo.

Kurejea kwa Yao na Abuya kunatoa ahueni kubwa kwa benchi la ufundi wakati timu ikijiwinda na mikikimikiki ya ligi pamoja na michuano mikubwa ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League).

Hali ya Majeruhi Wengine na Safari ya Pacome Zouzoua

Licha ya habari hizo njema, Kamwe amebainisha kuwa bado kuna wachezaji wanaoendelea na matibabu chini ya uangalizi maalumu, akiwataja Msalanga na Yusuf.

Kuhusu kiungo mshambuliaji kipenzi cha Wananchi, Pacome Zouzoua, uongozi umefafanua kuwa nyota huyo amesafiri kuelekea nchini Ufaransa kwa ajili ya awamu ya tatu ya matibabu na urekebishaji wa jeraha lake, baada ya awali kufanyiwa upasuaji nchini Tunisia.

“Unapofanyiwa upasuaji kama wa Pacome na kuanza kutembea, haimaanishi kuwa tayari umepona. Kuna mazoezi maalumu unayotakiwa kufanya. Siyo suala la kuanza kukimbia au kukanyaga mguu kidogo, kuna wataalamu na physio wenye weledi wa kukusaidia kurejea katika hali yako,” alisisitiza Ali Kamwe.

Kujali Maslahi ya Wachezaji

Kamwe aliongeza kuwa uongozi wa Yanga SC umegharamia kikamilifu safari na matibabu ya Pacome nchini Ufaransa kama sehemu ya utamaduni wa klabu hiyo kuwajali wachezaji wake wanapopata majeraha makubwa—utaratibu ambao uliwahi kutumika pia kwa aliyekuwa mshambuliaji wao, Yakuba Sogne.

Mashabiki wa Yanga sasa wanasubiri kwa hamu kuona mchango wa Yao na Abuya watakaporejea dimbani rasmi, huku wakimwombea Pacome apone haraka na kurejea kuendeleza makali yake.

Fadlu Davids: Yanga SC Hatutaki Robo Fainali Tena, Lengo Ni Ubingwa wa Afrika! Pigo Kubwa Yanga! Maxi Nzengeli Nje Wiki Sita, Hatari ya Upasuaji Yamnyemelea