Usajili wa Yanga dirisha
Yanga SC

Vita Kali! Yanga na Singida Black Stars Zagombea Saini ya Nyota wa Dodoma Jiji

Vardo November 23, 2026 11:10 am

Joto la usajili wa dirisha dogo la Januari 2027 limeanza kupanda mapema baada ya miamba ya soka nchini, Yanga SC na Singida Black Stars, kuingia vitani kuiwania saini ya kiungo mshambuliaji wa Dodoma Jiji, Khleffin Hamdoun.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani, vigogo hao wawili wamevutiwa na kiwango bora alichokionyesha nyota huyo tangu kuanza kwa msimu wa 2026/2027 akiwa na kikosi cha ‘Walima Zabibu’, hali iliyowafanya kuanza harakati za mapema za kuinasa saini yake.

Mkataba Wake Dodoma Jiji Uko Ukingoni

Hamdoun alijiunga na Dodoma Jiji Januari 12, 2026, akitokea Coastal Union kwa mkataba wa mwaka mmoja ambao unatarajiwa kufikia tamati Januari 2027. Hali hii inampa mchezaji huyo uhuru wa kufanya mazungumzo na klabu nyingine, ingawa uongozi wa Dodoma Jiji nao unapambana kumuongezea mkataba mpya wa mwaka mmoja zaidi.

Yanga Yaingilia Kati Mipango ya Singida

Inaelezwa kuwa tayari wawakilishi wa pande zote mbili wameanza mazungumzo na kiungo huyo. Hata hivyo, chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Singida Black Stars kimethibitisha kuwa kuingia kwa Yanga katika mbio hizo kumeongeza ugumu na ushindani mkubwa.

“Ni kweli Singida inafanya mazungumzo na mchezaji huyo lakini hakuna muafaka uliofikiwa hadi sasa, kwa sababu Yanga pia ni timu inayomfuatilia kwa ukaribu. Tunaendelea kufuatilia hadi mwisho kuona hali yake itakavyokuwa,” kilisema chanzo hicho.

Safari ya Kisoka ya Khleffin Hamdoun

Kiungo huyo mwenye uzoefu mkubwa na Ligi Kuu Bara ana historia ya kupita katika klabu kadhaa kubwa kabla ya kutua Dodoma:

  • Azam FC (2020): Alijiunga nayo Januari 8, 2020, akitokea Mlandege FC ya visiwani Zanzibar.

  • Muscat SC (Oman): Aliwahi kwenda kucheza soka la kulipwa nchini Oman kabla ya kurejea nchini.

  • Coastal Union (2025): Alijiunga na ‘Wagosi wa Kaya’ Septemba 8, 2025, kwa mkataba wa mwaka mmoja, lakini aliitumikia kwa miezi sita tu kabla ya kuhamia Dodoma Jiji Januari 2026.

Mashabiki wa soka sasa wanasubiri kuona ni kati ya Jangwani (Yanga) au Singida, wapi ambapo nyota huyo atatua mara tu dirisha dogo litakapofunguliwa rasmi Januari 2027.

El Mando Afunguka: Diamond, Nandy, Harmonize Walini-block Mitandaoni! FIFA Yaipa Ushindi Simba SC: Yanga Yamlipia Fadlu Davids Deni la Milioni 124!