ISHU YA CHAMA KUIBUKIA YANGA YAPAMBA MOTO, SIMBA WAJIBU KIVINGINE
IMEFAHAMIKA kuwa kiungo mchezeshaji raia wa Zambia, Clatous Chama, amekataa mkataba wa miaka miwili Simba wenye dau la Sh milioni 150 huku watani wao wa jadi wakimtengea Sh milioni 300. Kiungo huyo fundi, hivi karibuni ilielezwa amegomea mkataba wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea Simba huku akiwataka viongozi kusubiria hadi mkataba wake utakapomalizika mwishoni mwa msimu huu. Yanga hivi karibuni ilielezwa imeanza mazungumzo ya siri...
MBWANA SAMATTA: SINA NAMNA, NITAIKOSA TUNISIA
NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Samatta, atakosekana katika mchezo wa kwanza wa kufuzu fainali za kombe la mataifa ya Africa (AFCON) dhidi ya Tunisia kufuatia majeraha aliyoyapata wakati akitumikia klabu yake ya Fenerbahce ya Uturuki. Samatta amepata majeraha hayo siku ya Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Uturuki dhidi ya Klabu ya Konyaspor ambao ulimalizika kwa Fenerbahce kufungwa mabao 2-0. Akizungumzia majeraha hayo, Samatta amesema kuwa amefanyiwa vipimo anatakiwa...
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA ALHAMISI
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Spoti Xtra Alhamisi, lipo mtaani jipatie nakala yako jero tu
MAMBO MATATU YA KUFANYA ISHU YA SENZO WA YANGA KUSHIKILIWA NA POLISI
ANAANDIKA Saleh Jembe KATIKA hili suala la Senzo (Mbatha) na Mbaga (Hashim) kushikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za upangaji matokeo (match fixing) ni vizuri sana TUKAHESHIMU jeshi lenyewe na wahusika wenyewe.Kwanza:Senzo na Mbaga ni watuhumiwa, bado hawajahukumiwa na tuendelee kuwa na subira badala ya kuingiza ushabiki wa Uyanga na Usimba.Naona wengine wanawatetea na wengine wanawakandamiza. Vizuri tulipe nafasi...
TANZANIA U 20 YAAMBULIA KICHAPO CHA MABAO 2-1 DHIDI YA SUDAN
TIMU ya Taifa ya Tanzania, chini ya miaka 20 leo Novemba 11 imekubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya timu ya Taifa ya Sudan.Mchezo wa leo wa kirafiki umechezwa Uwanja wa Uhuru ambapo Sudan ilianza kufunga bao la kwanza dakika ya 10 kupitia kwa Mustafa Hassan dakika ya 10 na lile la pili lilifungwa na Nagigouma Alamin dakika ya...
MSHAURI WA YANGA, SENZO MATATANI KISA MATOKEO MABOVU YA SIMBA
IMEELEZWA kuwa aliyekuwa Mtedaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Senzo Mbatha anashikiliwa na Polisi katika kituo cha Oysterbay kwa tuhuma za kuihujumu Simba.Habari zimeeleza kuwa anahojiwa kuhusu ishu ya kudaiwa kuihujumu timu yake ya zamani ili ipate matokeo mabovu kwenye mechi za ligi zilizopita.Mbatha anadaiwa kufanya hivyo kwa kushirikiana na Hashim Mbaga, aliyekuwa mkurugenzi wa mashabiki na wanachama wa...
YANGA MZIGONI NOVEMBA 15, AZAM COMPLEX
BAADA ya kikosi cha Yanga kumalizana na Simba Novemba 7 Uwanja wa Mkapa kwa sare yakufungana bao 1-1 na wachezaji kupewa mapumziko kesho Novemba 12 wanatarajiwa kurejea kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon.Mchezo huo wa kirafiki unatarajiwa kuchezwa Novemba 15, Uwanja wa Azam Complex saa 1:00 usiku.Mchezo huo wa kirafiki ni maalumu...
SIMBA WAPO KWENYE HESABU ZA KUMVUTA NDANI KIUNGO HUYU MATATA
IMEELEZWA kuwa uongozi wa Simba upo kwenye mchakato wa kuongeza kiungo mkabaji ndani ya timu hiyo ambayo inaiwakilisha Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu wa 2020/21 na itaanza kibarua chake kati ya Novemba 27-29.Simba imepangwa kucheza na Klabu ya Plateu United kutoka Nigeria mchezo wa kwanza itakuwa ugenini na ule wa pili utachezwa Uwanja wa Mkapa kati...
PRINCE DUBE WA AZAM FC NA FAMILIA YAKE MAISHA YANAENDELEA
PRINCE Dube akiwa na familia yake nchini Zimbabwe ambapo ameitwa timu ya Taifa ya Zimbabwe.Nyota huyu anakipiga timu ya Azam FC vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 10.Kibindoni amefunga mabao sita na ana pasi nne za mabao.
WASHAMBULIAJI WAWILI STARS KUIKOSA TUNISIA
ADAM Adam mshambuliaji anayeongoza kwa mabao kwa upande wa wazawa katika Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa nayo 6 hakuambatana na timu ya Taifa ya Tanzania nchini Uturuki kutokana na kukosa pasi (Passport) ya kusafiria.Pia Nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta anayeichezea Klabu ya FC Fenerbahce ya Uturuki nae atakosekana katika kikosi cha Stars kitakachocheza michezo ya kufuzu Afcon 2021...