Uncategorized
YANGA YAFUNGUKA JUU YA KUMSAJILI NDEMLA
KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema kuwa kwa sasa hana mpango wa kumsajili kiungo wa Simba, Said Ndemla ambaye amekuwa akihusishwa kujiunga na kikosi chake.
Zahera amesema kuwa mpango wake ni kuwa na kikosi bora ambacho kitakuwa na ushindani msimu ujao kutokana na aina ya wachezaji ambao anawataka.
“Sina mpango wa kumsajili Said Ndemla, simjui huyo mchezaji na hayupo kabisa kwenye hesabu zangu.
“Nataka kufanya usajili ambao utakuwa na tija hivyo mashabiki wa Yanga watulie wasiwe na presha kila kitu kitakuwa sawa,” amesema.

Leave a Reply
You must be logged in to post a comment.