Timu ambayo ilikuwa inasubiriwa kushuka daraja kuungana na African Lyon imepatikana rasmi. Baada ya sintofahamu kutokea jana wakati ligi ilipomalizka. Stand United ya Shinyanga wameshuka daraja baada ya kufungwa na JKT Tanzania kwa goli 2-0 na JKT Tanzania, na kwa mujibu wa taarifa kutoka Bodi ya Ligi, na si Kagera Sugar tena.
Timu mbili ambazo zitacheza playoff (Michezo ya mitoano ) ni Kagera Sugar aliyeshika nafasi ya 18 na Mwadui FC aliyeshika nafasi ya 17.
Mwadui na Kagera watacheza na Pamba FC ya Mwanza na Geita Sports ya Geita. Mshindi wa playoff atapanda ligi kuu Tanzania bara msimu ujao tena
The post Ni Stand United, sio Kagera Sugar appeared first on Kandanda.