Home Uncategorized OBREY CHIRWA ATAKA KUREJEA YANGA

OBREY CHIRWA ATAKA KUREJEA YANGA


IMEELEZWA Kuwa baada ya mshambuliaji wa Azam FC, Obrey Chirwa kuigomea klabu hiyo kuongeza mkataba mpya ndani ya klabu hiyo ameanza mazungumzo na kikosi cha Yanga ili kujiunga nao msimu ujao.

Taarifa kutokana ndani ya Yanga zimeeleza kuwa Chirwa amekuwa akiwasiliana na viongozi wake wa zamani ili kuona namna gani anaweza kurejea tena kwenye kikosi chake cha zamani.

“Amekuwa akifanya mawasiliano na viongozi wa juu ili kurejea hapa Jangwani, unajua Chirwa kuna vitu anavikosa kule alipo ndio maana anadengua kuongeza mkataba,” kilieleza chanzo.

Akizungumza juu ya hatma ya Chirwa na Saleh Jembe, mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa wamekubaliana kusubiri mkataba wake uishe ili wakae mezani ikishindikana watamuacha.

“Chirwa ni mchezaji na anajielewa hivyo mkataba wake ukikamilika tutakaa naye mezani maana tulikuwa tunasubiri ligi iishe ndipo tujadili, kama atahitaji kuondoka itakuwa ni uamuzi wake,” amesema.

Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera aligoma kuzungumzia suala la kumrejesha Chirwa kwani awali alipotaka kujiunga na Yanga alimkataa waziwazi.

SOMA NA HII  VITA YA MANARA NA JERRY MURO YAREJEA TENA