Uncategorized

SAMATTA ATANGAZA KUREJEA SIMBA

admin May 30, 2019 9:09 pm


Straika tegemo katika timu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji, Mbwana Samatta, amesema kuwa endapo atamaliza harakati za maisha yake ya soka atarejea Tanzania kuungana na Simba.

“Wachezaji wengi wakubwa wanapokaribia kustaafu soka hurudi kwenye vilabu vyao vya zamani ambavyo viliwatoa.

“Nilikuwa mchezaji wa Simba zamani, hata nitakaporudi baadaye nafikiri nafasi ya kwanza itakuwa kwa Simba kwa sababu niliwahi kuitumikia lakini kama watakuwa hawanitaki ndio nitaangalia sehemu nyingine.
.
“Kwa heshima yao kwa sababu niliwahi kuwa mchezaji wao kwa hiyo nafasi ya kwanza lazima itakuwa kwao.”

EXCLUSIVE: USAJILI WA BIGIRIMANA WAZUA MSALA YANGA, APR KUCHUKA HATUA ZA KISHERIA HII SASA KAZI, AJIBU ATAKIWA NA BOSS WAKE KUTAJA SABABU ZINGINE ZA KUIKACHA TP MAZEMBE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply