Uncategorized

YANGA KUMALIZANA NA BEKI KISIKI WA KMC

admin May 30, 2019 9:34 am


IMEEELEZWA kwamba uongozi wa Yanga umeanza mazungumzo na beki wa kikosi cha KMC, Ally Ally ‘Mwarabu’ ili kupata saini yake msimu ujao.

Mwarabu amekuwa kiongozi ndani ya KMC na kuifanya safu ya ulinzi kuwa kisiki kwani KMC imekuwa ni namba moja kwenye timu zilizotoa sare nyingi ikiwa imefanya hivyo mara 16 msimu huu.

Habari zimeelezwa kuwa Yanga tayari wamefikia sehemu nzuri ya maelewano na beki huyo ambaye ni mwepesi akiwa ndani ya uwanja.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa suala la usajili lipo mikononi mwa kocha mkuu, Mwinyi Zahera hivyo kama jina lake lipo litafanyiwa kazi.

“kama jina lake lipo kwenye orodha ya mwalimu inawezekana tukazungumza naye ila kwa sasa hakuna taarifa kamili,” amesema.

ALLIANCE FC KUIFUMUA SIMBA NA YANGA YALIYOTOKEA MSIMU HUU YASIJIRUDIE KESHO, WACHEZAJI WAFUNDISHE ‘FAIR PLAY’ UWANJANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply