Kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Simba imeshindwa kuendelea kusikilizwa baada ya shahidi aliyeandaliwa kufiwa na kushindwa kufika mahakamani.
Kesi hiyo inawakabili hao waliokuwa viongozi wa Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange ‘Kaburu’ ambao wanakabiliwa na shitaka la kughushi na kutakatisha fedha huku Zachariah Hans Pope akiunganishwa katika kesi hiyo yeye kwa kudaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo za ununuzi wa nyasi bandia.
Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea leo Jumatatu kwa kusikilizwa ushahidi wa shahidi wa tano.
Wakili wa Serikali, Leonard Swai aliiambia mahakama kuwa tayari alikuwa ameandaa shahidi lakini alimpigia simu kuwa amefiwa mkewe hivyo ameshindwa kufika.
Hivyo Swai aliiomba mahakama kupangiwa tarehe nyingine kwa ajili ya kuendelea kusikilizwa kesi hiyo.
Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi, Thomas Simba alisema upande wa serikali uhakikishe kuwa unaanda mashihidi watatu ili akikosekana mmoja awekwe mwingine.
Swai ametakiwa kuleta mashahidi wengi watatu katika kesi hiyo ambayo inatarajiwa kuendelea Juni 12 na 13 mwaka huu.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.