Uncategorized

KESI YA JAMALI MALINZI YAPIGWA KALENDA

admin June 3, 2019 12:19 pm


MAHAKAMA imeshindwa kuendelea kusikiliza  kesi inayowakabili waliokuwa viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) baada ya Serikali kushindwa kuleta shahidi.

Kesi hiyo ilitarajiwa kuendelea leo Jumatatu ambapo shahidi wa 14 angetoa ushahidi wake kwenye kesi hiyo.

Wakili wa Serikali kutoka Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai aliiambia mahakama kuwa hakupata muda wa kuandaa mashahidi kwa kuwa alikuwa amesafiri hivyo apangiwe tarehe nyingine.

Hata hivyo wakili upande wa washitakiwa, Richard Rweyongeza aliiambia mahakama  upande wa Serikali wanatakiwa kutambua kuwa wateja wao wapo ndani hivyo ni vizuri kujipanga walau hata kuwa na mashahidi wawili ili kesi iweze kwenda.

Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Maira Kasonde alisema kuwa kesi hiyo imehairishwa mpaka Juni,10 mwaka huu.

MBADALA WA KINDOKI HUYU HAPA, ASAINI MIAKA MIWILI JANGWANI KESI YA AVEVA, KABURU, HANSPOPE YAKWAMA LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply