Uncategorized

MMOJA TEGEMEO YANGA ANASWA AZAM

admin June 5, 2019 11:54 am


INADAIWA beki kisiki wa Yanga, Andrew Vincent ‘Dante’ anawaniwa na mabingwa wa Kombe la Shirikisho (FA), Azam FC ambayo msimu ujao itashiriki Kombe la Shirikisho Afrika.

Dante amekuwa mmoja kati ya mabeki wa kati wa Yanga waliofanya vizuri msimu wa 2018/19 kwa kushirikiana na beki mkongwe Kelvin Yondani.

Habari za ndani zinadai kuwa nyota huyo anawindwa na Azam pamoja na timu nyingine kutoka nje ya Tanzania.

Hata hivyo, beki huyo inadaiwa bado Yanga inahitaji kubaki naye ili kuongeza nguvu kwenye safu ya ulinzi kwa msimu ujao.

Kwa upande wa Azam kupitia kocha Abdul Mingange, alisema: “Suala la usajili kwa sasa ni mapema kulizungumzia, ripoti yangu nitakabidhi kwa uongozi na kila kitu kitajulikana.”

CRISTIANO RONALDO HANA MPANGO WA KUSTAAFU TIMU YA TAIFA WANNE WAPANDISHWA KIZIMBANI KWA KUCHAPISHA MAUDHUI HASI YOUTUBE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply