Uncategorized

MWADUI WABISHI KINOMAA, WAIKOMALIA GEITA

admin June 8, 2019 3:20 pm

Salim Aiyee mshambuliaji wa Mwadui FC leo ameibuka shujaa baada ya kufunga mabao 2 ya ushindi yaliobakiza timu yake Ligi Kuu Bara.

Aiyee alianza kucheka na nyavu dakika ya 32 kabla ya Geita kusawazisha dakika ya 50 kupitia kwa Baraka Jerome.

Zikiwa zinahesabiwa sekunde kadhaa mchezo kuisha Aiyee aliwanyanyua mashabiki wa Mwadui FC kwa kupachika bao la pili dakika ya 90.

 Baada ya kupachika bao hilo Aiyee alivua Jezi hali iliyomlazimu mwamuzi kumuonyesha kadi ya njano.

Hivyo kwa matokeo hayo, Geita anarejea Ligi Daraja la Kwanza na Mwadui anarejea kwenye anga za TPL.

Timu za Ligi kuu msimu 2019/2020 hizi hapa BREAKING NEWS!! KAGERA SUGAR YASALIA LIGI KUU, MWADUI NAYO YACHEKELA DHIDI YA GEITA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply