Uncategorized

STARS YAPATA MAKOCHA WAWILI WAPYA, WAANZA KAZI MOJAKWAMOJA

admin June 11, 2019 2:21 pm

MWENDO Mdundo sasa kwa timu ya Taifa ya Tanzania ambayo imeweka kambi nchini Misri kwa ajili ya kujiaanda na michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza Juni 21.

Benchi la ufundi lililo chini ya Kocha Mkuu, Emmanuel Ammunike ameongezewa makocha wawili ambao wameongeza nguvu kwenye kambi hiyo na imeelezwa kuwa wamewahi kufanya kazi na Ammunike.

Makocha hao wote ni raia wa Misri wanaifanya timu hiyo kwa Sasa Stars kuwa na makocha sita, ambao kwa pamoja jukumu lao ni kuhakikisha wanapata matokeo chanya.

Taarifa ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), iliyotumwa na Ofisa Habari, Clifford Ndimbo imeeleza kuwa, makocha hao wameongezwa kwa mahitaji maalumu. 

“Kocha Abdelrahman Essa amebobea katika ujuzi wa mazoezi ya viungo wakati Ali Taha yeye ni mtaalamu mwenye ubobevu wa kutathmini kiwango,” ilisema taarifa ya Ndimbo.

Ikumbukwe kuwa Stars ni timu ya kwanza kutia timu Misri ipo kundi moja na timu ya Nigeria, Kenya na Senegal.

YANNICK CARRASCO KUIBUKIA KWA WASHIKA BUNDUKI KUBWA KULIKO NI YA KIBABE, MOJA KWA MOJA LITARUSHWA NA AZAM TV

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply