Uncategorized

KUBWA KULIKO NI YA KIBABE, MOJA KWA MOJA LITARUSHWA NA AZAM TV

admin June 11, 2019 3:26 pm

 Kubwa Kuliko itazinduliwa rasmi Jumamosi,Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga jijini Dar es Salaam na wanachama pamoja na viongozi wa Yanga lengo likiwa moja kuichangia timu.

Mchakato huo kwa mara ya kwanza ulizinduliwa na Kocha Mkuu, Mwinyi Zahera makao makuu ya nchi, Dodoma.

Katibu wa Kamati ya Hamasa ya Yanga, Deo Muta amesema kuwa maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika litaanza saa nne asubuhi hadi saa kumi kamili jioni.

Muta amesema kuwa, tamasha hilo linakwenda kuibadilisha Yanga na kutengeneza historia ndani ya timu hiyo katika kuhakikisha wanafikia malengo yao ya kujiendesha.

“Wadau mbalimbali tumewaarika katika tamasha hili kubwa la kihistoria la Kubwa Kuliko ambalo litafanyika kwa siku nzima ya Jumamosi hii wakiwemo wasanii wa Bongo Muvi na Bongo Fleva, wachezaji wa zamani, wanachama na mashabiki.


“Tamasha litakuwa ‘live’ likirushwa na kituo cha Televisheni cha Azam TV, pia kwa wale watakaokuwa mbali na TV, tumewarahishia kwa kuweza kuangalia kwa njia ya simu au ‘laptop’ kwa kutumia mfumo wa online wa ‘Pay Per View,”amesema Muta.

STARS YAPATA MAKOCHA WAWILI WAPYA, WAANZA KAZI MOJAKWAMOJA Wachezaji waliokamilisha usajili Ligi Kuu 2019/20

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply