UONGOZI wa Mtibwa Suar unesema kuwa msimu ujao wataboresha kikosi na kukifanya kiwe cha ushindani zaidi ya msimu uliomalizaka.
Akizungumza na Salehe Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kwa sasa wanapitia ripoti ya Kocha Mkuu Zuber Katwila.
“Msimu wa 2018/19 tulichechemea kidogo mwanzo ila kwa sasa tunajipanga kufanya makubwa zaidi msimu ujao, tunapitia ripoti kabla ya kuongeza wachezaji ama kupunguza,: amesema Kifaru.