Uncategorized

NYOTA WA BARCELONA AISHANGAA STARS, AIPA NAFASI YA KUFANYA MAAJABU AFCON

admin June 14, 2019 9:01 am


NYOTA wa zamani wa timu ya Barcelona, Chelsea, Inter Milan na timu ya Taifa ya Senegal, Samuel Etoo ameishangaa kuskia Tanzania inashiriki michuano ya Afcon mara baada ya kupita miaka 39.

Etoo amesema kuwa wakati anacheza na Senegal alipata bahati ya kucheza na kikosi hicho mara kadhaa lakini na aliona vipaji vingi kwa wachezaji wa Tanzania.

“Nimeshangazwa kuskia kwamba Tanzania inashiriki michuano ya Afcon baada ya kupita miaka mingi kushiriki kwani wakati nacheza na timu ya Tanzania nilikuwa napambana na wachezaji wenye vipaji.

“Ila kwa kuwa kwa sasa wamepata nafasi ya kushiriki naamini watafanya maajabu kwenye michuano ya Afcon kutokana na aina ya timu waliyonayo pamoja na vipaji ambavyo vipo Tanzania,” amesema Etoo.

Stars kwa sasa ipo nchini Misri ilipoweka kambi ambapo kazi kubwa ya maandalizi imeanza na jana walicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Misri na walipoteza kwa kufungwa bao 1-0.

KUMBE KILICHOMPONZA AIYEE ASIWIKE NI JERSON TEGETE NA KELVIN SABATO KUMEKUCHA NAMUNGO, WAGOMEA WACHEZAJI WA MAJARIBIO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply