WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt Harrison Mwakyembe, amewaomba Watanzania kuichangia Timu ya Taifa (Taifa Stars) ambayo ipo Misri kwa ajili ya michuano ya #AFCON2019
Mwakyembe amesema hayo leo Jumatatu, Juni 17, 2019 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu maandalizi ya Stars ykwa ajili ya fainali za AFCON.
“Siku ya Alhamisi asubuhi tutakuwa na zoezi kubwa ambalo litaluwa LIVE kwenye mitandao na television mbalimbali na kwenye radio ambapo tutafanya uchangiaji wa Taifa Stars. Nawahakikishia kila shilingi itakayopatikana itakwenda kwa vijana wetu, wasishindwe kwa kuvunjika moyo,” amesema.
Amesisitiza kwamba fedha zitakazochangwa si kwa ajili ya kuipeleka timu Misri na kuirudisha, “hatuhitaji kuwaweka kwenye hoteli nzuri (hayo yote yameshafanyika) tunahitaji kufanya kitu ili timu yetu ifanye vizuri.
“Leo hii Tanzania inajivunia kwamba ukitaja ma-striker wakubwa duniani huwezi ukamkosa Samatta, Mungu atupe nini? Ndiyo kipindi chetu, dunia sasa hivi inatambua Tanzania ipo mpaka hapa tulipofikia,” amesema Dkt. Mwakyembe.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.