Beki kiraka wa timu ya KMC, Ally Ally ‘Mwarabu’ amemalizana na uongozi wa Yanga kwa kusaini mkataba wa miaka miwili
Ally amekuwa bora ndani ya KMC hali iliyomvutia Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera na kuacha maagizo kwamba naye aongezwe kwa wachezaji wa ndani.
Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredirick Mwakalebela amesema kuwa mipango ya usajili inaendelea kwa sasa kwa wachezaji wa ndani kwani wale wa kigeni wamekamilisha maagizo ya mwalimu kwa asilimia 90.
SOMA NA HII KASI YA NYOTA MPYA WA SIMBA YAMKOSHA MBELGIJI WA SIMBA, ALICHOKIFANYA DAKIKA 12 NI BALAA