Kelvin John Mshambuliaji ambaye alikuwemo katika kikosi cha wachezaji 32 walioitwa na Amunike nchini Misri, amekiri kuwa kuwemo katika kikosi hicho kumemuongezea ujuzi na kumfungua zaidi, licha ya kutokuwemo katika kikosi cha wachezaji 23. Ameyasema hayo alipoongea na Michezo Leo ya Metro Fm.
“Nilitamani kuwa sehemu ya kikosi lakini sikubahatika kuwepo Mwalimu Yuko sahihi kwa kikosi alichokiteua kutuwakilisha Kwenye Mashindano ya Afcon kikosi kile Ni kizuri na kitatuwakilisha vizuri kikubwa Ni kuwaombea wachezaji wetu ili wafanye vizuri .
Alipoulizwa kuhusu kuondoka kwenda kucheza soka nje “Ni kweli Kuna Ofa nyingi ambazo Msimamizi wangu amezipokea na baada ya Timu kusikia nimeitwa Kwenye Timu ya Taifa imeniongezea thamani kubwa mpaka Sasa Nawezasema Kuna uwezekano wa asilimia 95 nikaondoka na kwenda klabu Moja wapo nje ya Tanzania”
Kelvin John alikuwa katika kikosi cha awali kilichoaanza maandalizi jijini Dar kabla ya kwenda Misri. “Nimejifunza Mambo mengi Kwenye kambi ya Timu ya Taifa Kutoka kwa Kaka zangu kubwa zaidi nidhamu kujituma na kutokata tamaa Mfano Samatta Baada ya majina 23 kutangazwa aliniita akaniambia usivunjike Moyo unamuda mrefu wa kucheza Taifa stars wewe ni Kijana mdogo endelea kupambana zaidi”
Kelvin amewahi kuongea na mtandao huu pia kuhusu nia yake ya kwenda kucheza nchini Ufaransa.
The post Kelvin John alitamani sana kubaki Misri appeared first on Kandanda.