Uncategorized

MAYANJA ATAJA SABABU ZA KUTUA KMC, ATAJA ATAKAOWASAJILI

admin June 26, 2019 12:33 pm

KOCHA mpya wa KMC, Jackson Mayanja amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya akubali kusaini klabu ya Halmashauri ya Kinondoni, KMC  ni mfumo wa klabu hiyo kumvutia na ubora wa kikosi.

Mayanja leo amesaini kandarasi ya mwaka mmoja kukinoa kikosi hicho ambacho kilikuwa chini ya Etiene Ndayiragije ambaye kwa sasa yupo Azam FC.

“Nimekubali kusaini KMC kwa kuwa ni klabu yenye mfumo mzuri wa uendeshaji hivyo nina imani tutafanya vema kwenye ushindani.

“Sina mpango wa kuja na wachezaji wangu ila ikipendeza nitakuja na mtu wa benchi la ufundi ili tusaidiane kwenye majukumu,” amesema.

Yanga, Kaseke wanazungumza kuhusu dili jipya VIDEO: MSIMAMO WA SERIKALI KUHUSU KAULI YA JAGUAR HUU HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply