Home Uncategorized Yanga, Kaseke wanazungumza kuhusu dili jipya

Yanga, Kaseke wanazungumza kuhusu dili jipya

YANGA SC bado wanahitaji huduma ya kiungo wa pembeni, Deus Kaseke ambaye mkataba wake unataraji kumalizika rasmi mwishoni mwa mwezi huu. Kaseke alijiunga Yanga kwa mara ya kwanza Juni, 2015 akitokea Mbeya City FC.

Alishinda mataji ya ligi kuu msimu wa 2014/15, 2015/16 na 2016/17 kabla ya kutimkia Singida United ya Singida msimu wa 2017/18 ambako aliisaidia timu hiyo iliyokuwa ikicheza ligi kuu kwa mata ya kwanza baada ya kusubiri miaka Zaidi ya 16 kufika fainali ya kombe la FA na kumaliza katika nafasi ya tano katika ligi kuu.

Alirejea Yanga Juni mwaka jana, na licha ya kuanza msiu akiwa mchezaji wa kikosi cha kwanza, Kaseke alijikuta nje ya kikosi baada ya Mrisho Ngassa kupewa nafasi kubwa Zaidi ya kucheza. Kulikuwa na taarifa kuwa kiungo huyo mshambulizi anaweza kujiunga na Namungo FC iliyopanda ligi kuu msimu huu, lakini Yanga nao wanahitaji kumbakisha mchezaji huyo ndiyo maana wamefungua mazungumzo.

“ Klabu bado inamuhitaji Kaseke, kocha pia anamtaka kuendelea kuwa nasi. Hakuwa na nafasi kubwa ya kucheza msimu uliopita lakini alionyesha kiwango kizuri kila alipopewa nafasi. “ kinasema chanzo cha habari hii ambacho kimeomba hifadhi ya jina lake.

“ Tunahitaji kubaki na wachezaji wetu bora hasa wale wa ndani na tunahitaji pia uzoefu wa wachezaji kama Kaseke ndani ya timu yetu. Kocha ameliona hilo ndiyo maana tunazungumza na Kaseke na tunaweza kufikia mwafaka kabla ya Jumatatu ijayo.”

The post Yanga, Kaseke wanazungumza kuhusu dili jipya appeared first on Kandanda.

SOMA NA HII  EXCLUSIVE!! YANGA YANASA KIFAA KUTOKA SIMBA