KIKOSI cha Simba ambacho kinaendelea kujiimarisha kwa ajili ya msimu mpya wa mwaka 2019-20 mpaka sasa tayari wamemalizana na wachezaji wa kigeni tisa kutoka mataifa tofauti.
Wachezaji hao watatu ni kutoka Brazili huku wengine wakiwa wanatoka ndani ya bara la Afrika kama ifuatavvyo:-
Meddie Kagere mshambuliaji wa Simba ameongeza mkataba wa miaka miwili yeye ni raia wa Rwanda na anakipiga pia timu ya Taifa ya Rwanda.
Clatous Chama, raia wa Zambia anayekipiga pia timu ya Taifa ya Chipolopolo ameongeza kandarasi ya miaka miwili yeye ni kiungo.
Sharaf Eldin Shoboub Ali Abdalrahman, kiungo raia wa Sudan amesaini kandarasi ya mwaka mmoja ametokea timu ya Al Hilal ya Sudan.
Wilker Henrique da Silva raia wa Brazil amesaini kandarasi ya miaka miwili ametokea Bragantino.
Gerson Fraga Veira ametokea ATK FC ya India yeye ni raia wa Brazil amesaini kandarasi ya miaka miwili.
Beki Tairone Santos da Silva raia wa Brazil amesaini kandarasi ya miaka miwili ametokea timu ya Atletico Cearense FC ya Brazil.
Sergio Wawa raia wa IvoryCoast yeye ni beki kisiki ndani ya Simba ameongeza kandarasi ya mwaka mmoja.
Deo Kanda yeye ni mshambuliaji raia wa Congo amesaini kandarasi ya mwaka mmoja
Francis Kahata yeye ni raia wa Kenya amejiunga na Simba kwa kandarasi ya miaka mwili akitokea timu ya Gormahia na anakipiga pia kwenye timu ya Taifa ya Kenya kwa nafasi ya kiungo.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.