Home Uncategorized BAADA YA KUPIGWA MKWARA NA ZAHERA, GADIEL MICHAEL NAYE ATOA MAAGIZO YANGA

BAADA YA KUPIGWA MKWARA NA ZAHERA, GADIEL MICHAEL NAYE ATOA MAAGIZO YANGA


Beki wa klabu ya Yanga, Gadiel Michael amesema yupo tayari kusaini Yanga mkataba mpya iwapo tu klabu hiyo itafikia dau na masharti ambayo amewapa, imeelezwa.

Taarifa imeeleza kuwa Gadiel amedai mpira ndiyo kazi yake hivyo amewapa mapendekezo viongozi wa klabu ya Yanga ili kusaini mkataba mpya.

Gadiel amefunguka kwa kusema kuwa, iwapo watashindwa mpaka tarehe 06 July atasaini klabu nyingine ambayo imekubali kumpa dau alilolitaka.

Tetesi za ndani zinasema tayari mchezaji huyo amefikia makubaliano na Simba ya kusaini mkataba wa miaka miwili.

SOMA NA HII  JEMBE LINGINE LINALOTAJWA KUMALIZANA NA SIMBA HILI HAPA